Ni hatari kutozima chombo cha moto ukiwa sheli
4 June 2024, 10:08 am
Usalama dhidi ya moto ni pamoja na madereva wa vyombo vya moto kujua na kuzingatia maelekezo yakuzima vyombo vyao vya moto wanapokuwa katika vituo vya kuongezea mafuta.
Na Majabu Madiwa
Waendeshaji wa Vyombo vya Moto Wilaya ya Pangani wametakiwa kuzima vyombo vyao wanapofika katika Vituo vya kujazia mafuta ili kuepusha uwezekano wa kusababisha mlipuko.
Wito huo umetolewa na Staff Sajenti Musa Msengi kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati wa Mafunzo ya Uzimaji Moto na Uokozi kwa wafanyakazi wa Shirika la Uzima kwa Sanaa (UZIKWASA) lenye makao yake wilayani Pangani.
Msengi amesema ni vyema waendeshaji wa Vyombo vya moto wakazingatia kanuni na maelekezo wanayopewa kwenye Vituo vya Mafuta ili kuepusha majanga ya moto.
Aidha amezungumzia shutma zinazoelekezwa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuchelewa kwenye matukio na Magari yake kukosa maji.