Tenki lazuia michango ya chakula shuleni
8 May 2024, 10:26 pm
Kabla ya mwezi wa pili zoezi la kuchangia chakula cha shule ya msingi Bushiri lilikuwa likiendelea vizuri na kufikia idadi ya wazazi 200 lakini baada ya kuibwa kwa tenki hilo idadi imepungua kufikia 40.
Na Cosmas Clement
Hayo yamesemwa na wajumbe wa kamati ya Urakhibishi wa kijiji cha Msaraza, wakati wa uwasilishaji wa changamoto zilizoibuliwa na wananchi wa kijiji hicho.
Akijibia suala hilo afisa mtendaji kata ya Bushiri bwana Mwinyimkuu Sultan amesema changamoto ya kuibwa kwa tenki inaendelea kufuatiliwa kupitia vyombo vya sheria huku akiwaasa wanakamati hao kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuchangia chakula
Naye mwenyekiti wa kijiji cha Msaraza Salimu Mazika amewaasa wajumbe wa kamati hiyo kupeleka elimu kwa jamii za wafugaji kijijini hapo ili kupunguza kiwango cha utoro katika shule hiyo.
Kikao hicho kimewakutanisha wajumbe wa kamati ya Urakhibishi wa kijiji cha Msaraza, viongozi wa kijiji hicho na pamoja na Mkurugenzi wa Asasi ya usaidizi wa Kisheria Pangani (PACOPA) na Mratibu wa Urakhibishi Pangani.