Pangani FM
Pangani FM
27 March 2026, 13:50

“Hapa kwetu tuna vituo 33 vya kutolea matibabu ya afya ya akili, ambavyo vinajumuisha vituo vyote vya kutolea huduma za afya kuanzia ngazi ya Zahanati hadi hospital“
Na Mwandishi Wetu
Wananchi katika wilaya ya Tanga, mkoani Tanga wameaswa kuepuka kutumia majina yanayowanyanyapaa wenye changamoto ya matatizo ya afya ya akili kwani ni matatizo yanayoweza kumpata mtu yoyote.
Hayo yamesemwa na Mratibu wa afya ya akili Jiji la Tanga Dkt George Semsela, kufuatia uwepo wa baadhi ya watu kutumia maneno potofu dhidi ya watu wenye matatizo ya afya ya akili.
Amesema changamoto ya matatizo ya afya ya akili ni kubwa huku akielezea idadi ya watu waliohudhuria hospitali kwa ajili ya changamoto hiyo.
Amewasihi wanajamii kuondokana na mitazamo ya imani za kishirikina juu ya changamoto ya afya ya akili na kuchukua hatua madhubuti kujiupusha na vihatarishi vinavyopelekea matatizo hayo.