Pangani FM

Pangani yajidhatiti kudhibiti TB

24 March 2026, 22:04

Picha kuhusu ugonjwa wa Kifua kikuu

Wataalamu wa afya katika zahanati na vituo vya afya wilayani Pangani watakuwa wakipima watu wanaohisiwa kuwa na dalili za Ugonjwa wa kifua kikuu ili waanzishiwe dawa mapema pale watakapo bainika.

Na Saa Zumo

Wakati dunia ikiadhimisha siku kifua kikuu hii leo March 24,2026, katika wilaya ya Pangani Kata za KIPUMBWI na MKALAMO wilayani Pangani mkoani tanga zatajwa kuongoza kuwa na maambukizi ya kifua kikuu hali inayopelekea wilaya hiyo kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na ugonjwa huo.

Hayo yameelezwa na ABDALLAH AHMED USSI mratibu wa Kifua kikuu na Ukoma Wilayani Pangani na kutaja kundi linaloongoza kuwa na maambukizi hayo kuwa ni Wazee na watoto.

sauti ya dkt USSI

Dokta Ussi amewashauri Wataalamu wa afya katika zahanati na vituo vya afya wilayani Pangani kupima watu wanaohisiwa kuwa na dalili za Ugonjwa wa kifua kikuu ili waanzishiwe dawa mapema pale watakapo bainika.

Sauti ya Dkt Ussi

Katika mapambano dhidi ya kifua kikuu nchini dokta Ussi amewaomba wadau kuunga mkono wahudumu wa afya ngazi ya jamii ili kuwapo motisha ya kuendelea kufanya kazi hiyo kwa ufanisi.

Sauti ya Dkt Ussi

Kauli mbiu ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani 2026 ni “Ndiyo! Tunaweza kumaliza TB!”kauli hii inaonyesha matumaini ya kimataifa na kujitolea kwa kutokomeza kifua kikuu.

Na Inasisitiza kwamba kukomesha kifua kikuu kunawezekana kwa hatua madhubuti na ushirikiano.