Pangani FM

Pangani kuvunja rekodi upandaji miti

17 March 2026, 19:19

Miche ya miti ikiwa katika viriba: Picha Tovuti ya TFS

Halmashauri ya Wilaya ya Pangani imesema inatarajia kuvuka lengo la serikali la kupanda miti mil. 1.5  mwaka huu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha Wiki ya Upandaji Miti Duniani ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Na Cosmas Clement

Akizungumza na Pangani FM kwa njia ya simu Mkuu wa Idara ya Maliasili na Mazingira Bw. Twahiru Mkongo amesema kuelekea wiki hiyo wamepanga kufanya zoezi la upandaji miti katika shule ya msingi Bushiri kwa kupanda miti zaidi ya 500.

Mkuu wa Idara Maliasili na Mazingira Twahiru Mkongo

Bwana Mkongo amesema mpaka sasa wilaya kwa kushirikiana na wadau wamefanikiwa kupanda miti zaidi ya milioni moja aina ya mikoko.

Mkuu wa Idara Maliasili na Mazingira Twahiru Mkongo

Hatua hiyo inakuja katika kuekeleza kilele cha Wiki ya Upandaji Miti Duniani ambapo tayari wilaya ya Pangani imesambaza miche ya miti mbalimbali katika vijiji vilivyopo wilayani humo.