Pangani FM

Wananchi waaswa kutofanya shughuli za kiuchumi karibu na vyanzo vya maji

17/03/2026, 19:03

Mkurugenzi wa bodi ya bonde la mto Pangani Bwana Segule A. Segule

Na Cosmas Clement

Wananchi wa wilaya ya Pangani na maeneo yanayozungukwa na bonde la mto Pangani wametakiwa kulinda vyanzo vya maji kwa kuacha kufanya shughuli za kibinadamu karibu na kingo za mto na maeneo ya vyanzo vingine vya maji.

Hayo yamezungumzwa na Mkurugenzi wa bodi ya bonde la mto Pangani Bwana Segule A. Segule wakati akizungumza na Pangani FM kwa njia ya simu, ambapo amesema wananchi wanaposhiriki katika ulinzi vyanzo vya maji itasaidia kupata uendelevu wa huduma ya maji.

Sauti ya Mkurugenzi Segule

Amesema ofisi ya bodi ya bonde la Mto Pangani inaitumia wiki ya maji kwa kujitathimini hivyo milango ipo wazi kwa wadau wa maji kutoa mapendekezo ili kuendeleza vyanzo vya maji na kutoa huduma bora ya upatikanaji wa maji.

Sauti ya Mkurugenzi Segule

Kuhusu kaulimbiu ya mwaka huu ya Maji na Jinsia Bwana Segule amesema inalenga kuleta usawa katika matumizi na kulinda vyanzo vya maji kwa manufaa endelevu.

Sauti ya Mkurugenzi Segule

Siku ya maji Duniani, mwaka 2026 inaadhimishwa Machi 22 ikibebwa na kaulimbiu ya “Maji na Jinsia inalenga kuangazia usawa katika upatikanaji wa huduma za maji na Rasilimali za Maji na kugharamia masuala ya Jinsia katika kuandaa na kutekeleza Miradi.