Pangani FM

Rushwa yakwamisha kesi wilayani Handeni

17/03/2026, 12:34

Baadhi ya wanakamati ya MTAKUWWA wa kata Kabuku wilayani Handeni wakiwa katika mafunzo

Na Saa Zumo

Rushwa inatajwa kuchangia kukwamisha kesi za ukatili wa kijinsia  kata ya Kabuku Wilayani Handeni mkoani TANGA.

Hayo yamezungumzwa na baadhi ya wajumbe wa kamati zya MTAKUWWA kata ya Kabuku wilayani Handeni ambapo wamesema wanakumbana na ugumu wa kutokomeza changamoto ya matukio ya ukatili kutokana na wahalifu wa vitendo vya ukatili kutajwa kutoa Rushwa ili kesi zisiendelee.

sauti ya wajumbe wa kamati ya mtakuwwa

Ili kufanikisha mapambano dhidi ya kushughulikia kesi za ukatili katika eneo la Kabuku wajumbe wameshauriwa kutunza siri ili kufanikisha utatuaji wa matukio hayo.

Sauti ya wajumbe wa mtakuwwa Kabuku

Mmoja kati ya mjumbe ambaye ni mwalimu katika shule ya sekondary katika kata hiyo amesisitiza jamii kutenga muda wa kuwasikiliza watoto ili kutambua changamoto zinazowakabili.