Pangani FM
Pangani FM
04/03/2026, 20:33

Na Saa Zumo
Mmomonyoko wa maadili katika jamii wilayani Pangani unatajwa kuwa chanzo cha uwepo wa Mimba za utotoni kwa wasichana.
Hayo yameeleza na Mkaguzi wa Polisi na mkuu wa dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Pangani Inocent Panga wakati akizungumza na kituo hiki kuelekea siku ya mwanamke duniani March 8 2026.
PANGA amesema baadhi ya wazazi hawatimizi wajibu wao katika malezi ikiwemo kuwaelezea watoto wao wa kike mabadiliko ya Kimwili na kuwaacha kukumbana na changamoto katika ukuaji wao.
Kaulimbiu ya maadhimisho ya Siku ya mwanamke duniani mwaka 2026 ni “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi kufikia Dira 2050”
Ambapo Afisa kutoka kutoka dawati la jinsia na watoto Pangani Chali Haji amezitaja haki zinazopigiwa chepuo katika maadhimisho hayo kwa mwaka huu 2026.
Maadhimisho ya SIKU ya kimataifa ya wanawake mwaka huu yanajengwa juu ya misingi ya Ulingo wa Beijing wa mwaka 1995 unaolenga kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake kupitia ajenda 12 muhimu, ikiwemo kupinga umaskini, ukatili wa kijinsia, kuboresha afya na elimu, pamoja na kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi na uchumi.