Pangani FM
Pangani FM
04/03/2026, 20:18

Na Saa Zumo
Takribani kesi 5 za Usambazaji wa video za ngono zimeripotiwa tangu January hadi March 2026 katika kitengo cha Dawati la jinsia na watoto Jeshi la Polisi Wilayani Pangani.
Hayo yameelezwa na Afisa kutoka dawati la jinsia na watoto Pangani Chali Haji wakati akizungumza na kituo hiki ikiwa ni kuelekea kilele cha Siku ya Kimataifa ya Wanawake kwa mwaka huu.
Amesema katika usambazaji wa Video hizo waathirika wa kuu ni Wanawake ambapo kwa mujibu wa sheria ya makosa ya mtandao ni kila anayehusika kusambaza anaingia katika mikono ya sheria pale atakapo bainika.
Kwa upande wake Aneth Biabatho kutoka Dawati la jinsia na watoto Wilayani Pangani amesema vyanzo vya usambazaji wa video hizo ni wanawake huku elimu ikihitajika ili kukomesha vitendo hivyo ambavyo vimekuwa vikileta madhara kwa jamii.
Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka 2026 ni “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi kufikia Dira 2050”, ikilenga kujenga uelewa wa kuwekeza katika maendeleo jumuishi kwa kutambua na kutekeleza haki za wanawake na wasichana kwa vitendo.