Pangani FM

Uongozi wa Mguso wawafungua MTAKUWWA Mkata

19 February 2026, 6:35 pm

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA kata ya Mkata wilayani Handeni wakiwa katika mafunzo ya Uongozi wa Mguso.

“Mafunzo haya yameniwezesha kukumbuka majukumu yangu katika kamati hii ya MTAKUWWA hivyo nilichokipokea ni kujitathimini na pia kuwa na mshikamano kwa ajili ya kwenda kupinga ukatili katika maeneo yetu” Wajumbe wa MTAKUWWA Mkata

Na Cosmas Clement

Wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA kata ya Mkata wilayani Handeni wamesema mafunzo ya uongozi wa mguso yanayotolewa na shirika la Uzima kwa Sanaa (UZIKWASA) yamewawezesha kutambua majukumu yao katika kushughulikia matukio ya ukatili.

Hayo wameyasema katika siku ya kwanza ya mafunzo hayo yanayotolewa kwa siku mbili ambapo katika siku hiyo wameweza kuainisha changamoto zilizopo katika kata yao pamoja na kueleza majukumu yao ya kamati ya MTAKUWWA.

Wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA kata ya MKATA

Akielezea kuhusu lengo la mafunzo hayo, mwezeshaji kutoka shirika la Uzima kwa sanaa (UZIKWASA) bwana Joseph Peniel amesema ni mkakati wa shirika hilo kuzipa uwezo kama za MTAKUWWA katika maeneo mbalimbali ya nchi kuwa na uwezo wa kuchukua hatua dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Sauti mwezeshaji kutoka Uzima kwa Sanaa

Mafunzo hayo ya uongozi wa mguso kwa kamati ya MTAKUWWA kata ya Mkata wilaya ya Handeni ni muendelezo wa afua za shirika la Uzima kwa Sanaa kuzipa uwezo kamati za MTAKUWWA zilizoundwa na serikali katika maeneo mbalimbali ya nchi.