Pangani FM

Jinsi vyeo, nafasi za uongozi zinavyoumiza wananchi

17 February 2026, 6:26 pm

Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya uongozi wa mguso yanayotolewa shirika la UZIKWASA katika Halmashauri ya Handeni: Picha Sophia Mwilawa Handeni DC.

Mimi baada ya mafunzo haya nitakaa na vijana wangu pale ofisi ili niwaeleze njia sahihi za matumizi ya vyeo na nafasi zetu

Na Cosmas Clement

Matumizi yasiyo sahihi ya vyeo na nafasi kwa viongozi vimetajwa kuwa miongoni mwa mikwamo ya kutoa huduma bora kwa wananchi wanawaongoza.

Hayo yamesemwa na washiriki wa mafunzo ya uongozi yanayotolewa na shirika la UZIKWASA kwa wakuu wa idara na vitengo wa halmashauri ya Handeni kwa lengo la kuwawezesha kutumia mbinu wezeshi katika kutatua changamoto za kijamii na kuimarisha mahusiano ya na jamii.

Katika mafunzo hayo washiriki waliwezeshwa katika kufahamu matumizi sahihi ya vyeo na nafasi pamoja na tathimini binafsi hivyo kuwawezesha kugundua maeneo ya kufanyia kazi.

Sauti ya washiriki wa mafunzo
Washiriki wa mafunzo ya Uongozi wa Mguso

Kwa upande wake meneja wa ufuatiliaji na tathimini na mwezeshaji wa shirika la UZIKWASA bwana Joseph Peniel amesema kupitia mafunzo hayo wanatarajia kuona mabadiliko ya kiutendaji kwa washiriki hao wa mafunzo.

Sauti ya Joseph Peniel kutoka UZIKWASA

Mafunzo ya uongozi wa Mguso kwa wakuu wa idara na vitengo wa halmashauri ya wilaya ya Handeni yameanza leo na yanatarajiwa kuhitimishwa kesho.