Pangani FM

Jinsi bahari ya Pangani inavyokula watu

9 December 2025, 1:41 pm

Katika bahari ya Pangani kumekuwa kukishughudiwa ajali za watu kuzama na kufa maji kila mwaka wakiwa wanaogelea ama kusafiri.

“Wazazi wanapaswa kuwalinda watoto wao kuhakikisha hawafiki katika maeneo ya hatari wakati wa kuogelea”

Na Hamisi Makungu

Watoto wawili wenye umri wa miaka 13 hadi 14 wamepoteza maisha siku ya Jumatatu jioni wakiwa wanaogelea katika Bahari ya Hindi hapa Wilayani Pangani.

Watoto hao ambao wote ni wakiume, mmoja ametambuliwa kwa majina ya Nasri Ally Kassiun na mwengine ametambuliwa kwa jina moja la Shaibu.

Miili ya watoto hao imefikishwa jana jioni katika Hospitali ya Wilaya ya Pangani, baada ya jitihada za kuopoa miili hiyo kufanikiwa.

Akizungumza na Pangani FM Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitalini hapo Dkt. Nickson Patrick amethibitisha Hospitali hiyo kupokea miili ya watoto hao ikiwa tayari katika hali ya umauti.

Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitalini hapo Dkt. Nickson Patrick

Mwenyekiti wa kitongoji cha Funguni Kijiji cha Pangani Mashariki Bwana Yasri Salum amesema tukio hilo ni la tano kwa mwaka huu, hivyo amewataka wazazi kuwa makini katika malezi ya watoto wao hasa kipindi hiki cha likizo na msimu huu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Funguni Bwana Yasri Salum

Awali Pangani FM imezungumza na Bi. Mwamvita Hassani Mwinyi mmoja ya mashuhuda kwenye tukio hilo.

Shughuda wa tukio