Pangani FM

Wazazi waaswa kuwa macho ukatili wa watoto nyumbani

26 June 2025, 9:54 am

Katibu Tawala wilaya ya Pangani Esta Zulu Gama

Nalipongeza shirika la UZIKWASA kwa kutoa elimu kwa jamii juu ya masuala ya ukatili wa kwa wanawake na watoto, jamii kila mtu awajibike katika nafasi yake katika hili.

Na Cosmas Clement

Wazazi na walezi wilayani Pangani mkoani Tanga wametakiwa kusimama ipasavyo katika wajibu wa kulea na ulinzi wa watoto wao ili kuwaepusha dhidi ya vitendo vya ukatili.

Wito huo umetolewa na katibu tawala wilaya ya Pangani Esta Zulu Gama wakati akizungumza katika kikao maalumu kilichowakutanisha viongozi wa kada mbalimbali wilayani humo na shirika la UZIKWASA.

sauti ya katibu tawala wilaya ya Pangani Esta Zulu Gama

Pia amewaasa viongozi wa dini kutumia mahubiri kuonya juu ya vitendo vya ukatili ili kupunguza matukio hayo wilayani Pangani na kujenga jamii iliyo bora.

sauti ya katibu tawala wilaya ya Pangani Esta Zulu Gama
Baadhi ya washiriki wa kikao maalumu cha shirika la UZIKWASA na wadau wa masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto

Aidha ameipongeza shirika la UZIKWASA kwa kutoa elimu ya kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wilayani Pangani.

sauti ya katibu tawala wilaya ya Pangani Esta Zulu Gama