Pangani FM

Wananchi Pangani kuupokea mwenge wa uhuru Juni 14

13 June 2025, 7:08 pm

Picha ya mkuu wa wilaya ya Pangani Mhe. Gift Isaya Msuya. Piacha na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Pangani

“Napenda kuwaasa wananchi wa Pangani kujitokeza kwa wingi tarehe 14 juni kuupokea mwenge wa uhuru utakapopita katika maeneo yao”

Na Cosmas Clement

Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Mheshimiwa Gift Isaya Msuya, amewaasa wananchi wote wa Wilaya ya Pangani kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mapokezi ya mbio za Mwenge wa Uhuru zitakazofanyika tarehe 14 Juni 2025 katika viwanja vya Shule ya Msingi Mwembeni.

Ametoa rai hiyo jana, na kubainisha kuwa, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika miradi mbalimbali na utatumika kukagua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika vijiji vya Mwembeni, Pangani Mashariki, Pangani Magharibi, na Mikocheni.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Pangani Gift Msuya

Pamoja na uzinduzi wa miradi hiyo, Mheshimiwa Msuya amesema Mwenge wa uhuru utapitia kukagua masuala mtambuka.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Pangani Gift Msuya