Pangani FM
Pangani FM
9 June 2025, 9:21 pm

Matukio ya kufa majini hutokea katika bahari ya hindi mjini Pangani nyakati za sikukuu, na mara nyingi vifo hivyo hutokea kwa wageni wanaojaribu kuogelea kwa mara ya kwanza katika eneo hilo.
Na Rajabu Mrope
Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 16 mkazi wa Muheza amefariki baada ya kuzama maji katika eneo la Pangadeko mjini Pangani mkoani Tanga.
Akizungumza kwa njia ya simu na Pangani Fm mwenyekiti wa kitongoji cha Funguni Yasri Salim amesema tukio hilo limehusisha watu wawili kuzama wakati sikukuu ya pili ya Eid El Adha huku mmoja akiokolewa akiwa hai.

Mwenyekiti pamoja na kuelezea tahadhari zilizokuwepo katika eneo la fukwe hizo,amewataka watu wanaokuja kuogelea kwenye eneo waweze kuwasiliana na viongozi wa Kijiji ili kupata maelezo juu ya maeneo ambayo ni hatari kuogelea.