Pangani FM
Pangani FM
5 June 2025, 7:13 pm

“Kamati zilizopita zilikuwa hazina mahusiano mazuri na wavuvi hivyo ilikuwa ni ngumu kufikia lengo“
Na Majabu Madiwa
Kamati ya BMU ya Kijiji cha Ushongo Wilayani Pangani Mkoani Tanga imeeleza kujivunia kuwezesha mahusiano Chanya baina kamati na wavuvi tofauti na hapo awali.
Hii ni baada ya kamati hiyo kueleza utofauti wa kiutendaji kwa kamati ya sasa ikiwemo kuwashirikisha wanawake katika masuala ya utunzaji na uhifadhi wa mazingira ya fukwe na Bahari na kuongeza mawasiliano na mshikamano na wavuvi.
Bwana Mungia Mgaza ni mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Ushongo anaeleza namna ushirikiano unavyowezesha majadiliano baina ya wavuvi,kamati ya BMU,uongozi wa serikali ya Kijiji na wananchi hasa katika kufanikisha zoezi la ufungiaji wa mwamba.
Bw Salimu Mohamed katibu wa BMU katika Kijiji cha Ushongo amesema kamati zilizopita zilikuwa hazina mahusiano mazuri na wavuvi hivyo ilikuwa ni ngumu kufikia lengo huku akieleza namna kamati ya BMU ya sasa ilivyowezesha mahusiano na mawasiliano baina yao akiyataja mafunzo ya uongozi wa mguso yanayotolewa na shirika la Uzikwasa Wilayani Pangani kuchangia katika kufikia hatua hiyo.