Pangani FM

MKUBA yaivuruga mikopo ya kausha damu

5 June 2025, 6:41 pm

Aliyesimama Bi Sara Kwirini afisa maendeleo kata ya Bweni. Picha na Cosmas Clement

MKUBA ni kifupi cha neno Mfuko wa Kutunza Bahari inawawezesha wananchi wa kikundi cha mfuko huo kutunza akiba na kukopa na kurejesha.

Na Cosmas Clement

Uwepo wa vikundi vya Mfuko wa kutunza Bahari (MKUBA) katika vijiji vya Bweni na Ushongo wilayani Pangani Mkoani Tanga, umetajwa kuwawezesha wananchi wa vijiji hivyo kuondokana na mikopo umiza hivyo kuboresha vipato vyao.

Hayo yamebainishwa na wanachama wa vikundi hivyo kupitia risala yao walioiwasilisha mbele ya mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa vikundi vya MKUBA vya kijiji cha Bweni na Ushongo uliofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Kikokwe hii leo.

Pamoja na hayo wajumbe hao wamesema mkuba imewasaidia kutunza mazingira ya koko na fukwe na kupunguza changamoto za mikopo umiza.

sauti wa mjumbe wa mkuba bweni akisoma risala

Kwa upande wake mratibu wa MWAMBAO mkoa wa Tanga, Bwana Ahmad Salum, amewapongeza wajumbe wa MKUBA kwa jitihada walizozifanya kwa kuboresha mitaji yao.

Sauti ya mratibu wa mwambao Tanga Bwana Ahmad Salum
Mratibu wa mwambao Tanga Bwana Ahmad Salum. Picha na Cosmas Clement

Naye Bi Sara Kwirini Afisa Maendeleo kata ya Bweni ambaye alimwakilisha mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Pangani Bi Sekela Mwalukasa, amewaomba wananchi kuhamasika kujiunga na vikundi vya MKUBA ili kujikomboa kiuchumi.

Sauti ya bi Sara Kwirini

Mradi wa mfuko wa kutunza bahari unaendeshwa na taasisi ya Mwambao unawawezesha wanajamii kukoba akiba zao za kikundi na kurejesha bila ya riba.