Pangani FM

Jinsi nyuki wanavyolinda misitu wilayani Pangani

27 May 2025, 11:44 am

Ufugaji wa nyuki. Picha Kutoka Mtandaoni

“Tumeanzisha ufugaji wa nyuki ili kulinda msitu wetu, nyuki ana kipato kuliko kukata mti na kuchana mbao au mkaa.”

Na Cosmas Clement

Kijiji cha Mtonga kilichopo wilayani Pangani ni miongoni mwa vijiji vilivyoathiriwa na shughuli za ukataji wa misitu kwa ajili ya shughuli uchomaji wa mkaa na upasuaji wa mbao.

Ili kukabiliana na changamoto hizi, juhudi mbalimbali zimeanzishwa, ikiwa ni pamoja na utoaji wa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kuhifadhi misitu na vyanzo vya maji, pamoja na ushirikiano kati ya serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kama UZIKWASA katika kuhamasisha uhifadhi wa mazingira.

Kufuatia juhudi hizo mafunzo ya mazingira yalitolewa kwa kamati hiyo, hivyo kuwezesha wanakamati kuja na wazo la ufugaji nyuki, je ni jinsi gani inawasiadia kulinda msitu wao ?

Karibu, kusikiliza makala hii.