Pangani FM

Pangani yajipanga kumpokea Dkt. Samia

4 February 2025, 1:36 pm

Katibu tawala wilaya ya Pangani Bi Esta Zulu Gama aliesimama akizungumza na madiwani na watumishi waliohudhuria katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Pangani.

Ni mara ya kwanza kwa Dr. Samia Suluhu Hasan kutembelea wilaya ya Pangani tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Na Maajabu Madiwa

Watumishi Wilayani Pangani Mkoani Tanga wameaswa kutoa huduma kwa kukidhi maratajio ya wananchi.

Rai hiyo imetolewa na Bi Esta Zulu Gama katibu Tawala Wilayani Pangani katika Mkutano wa baraza la madiwani la robo ya pili ya Oktoba -Disemba uliofanyika hii leo huku kamati mbalimbali zikiwasilisha taarifa za utekelezaji wa shughuli zake.

sauti Katibu Tawala wilaya ya Pangani

Pamoja na hilo Bi Esta akatoa taarifa ya ujio wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hasan anaetarajiwa kufanya ziara mwezi February mwaka huu Wilayani Pangani.

sauti Katibu Tawala wilaya ya Pangani

Kwaupande wake mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Pangani Mh AKIDA BAHORERA mbali na kuwashukuru wataalam na madiwani kwa namna wanavyochechea maendeleo akatoa sisitizo la kushughulikiwa kwa changamoto zinazolalamikiwa na wananchi ikiwemo eneo la afya.

Sauti ya mhe. Bahorera