Pangani FM

Wanawake waongoza kwa magonjwa yasiyoambukiza Pangani

13 November 2024, 12:16 pm

Tumeona tuongelee magonjwa ya kisukari na pressure ya juu kutokana na magonjwa haya kuongezeka kwa kasi katika jamii yetu ya Pangani

Na Hamis Makungu

Mtindo wa Maisha usiofaa umeendele kuchangia ongezeko la Magonjwa yasiyoambukiza hasa kwa wanawake Wilayani Pangani.

Akizungumza na Pangani FM Mratibu wa Magonjwa yasiyoambukiza Dokta Rashidi Mahmud Makoko amesema ulaji usiofaa na tabia bwete zinachangia kuongezeka kwa wagonjwa wa kisukari na shinikizo la juu la Damu, hasa kwa wanawake.

Ili kukabiliana na Magonjwa hayo, ameshauri jamii hasa wanawake kufanya mazoezi na kubadili mtindo wao wa Maisha, sambamba na kujenga tabia ya kuchunguza afya mara kwa mara.

Sauti ya mratibu wa magonjwa yasioambukiza (W) Pangani Dokta Rashid Makoko

Kwa upande wake Dokta Abdallah Simba mbali na kuzitaja dalili za Magonjwa hayo na athari zake, amesema watu wengi wanasumbuliwa na Magonjwa yasiyoambukiza na hawajitambui.

Sauti ya Dokta Abdallah Simba kutoka (W) Pangani

Maadhimisho ya Kitaifa Wiki ya Magonjwa yasiyoambukiza yaliyoanza tarehe 9 na kwenda hadi tarehe 16 Novemba Mwaka huu yamebebwa na Kauli Mbiu isemayo “Muda ni sasa, Zuia Magonjwa yasiyoambukiza Mahali pa Kazi”