REA yahamishia nguvu vitongojini Pangani
25 October 2024, 9:03 pm
Utekelezaji wa usambazaji wa umeme katika vitongoji kumi na tano wilayani Pangani unatarajiwa kukamilika mwaka wa fedha ujao.
Na Cosmas Clement
Serikali kupitia REA inatarajiwa kutekeleza mradi wa Usambazaji wa umeme katika vitongoji kumi na tano wilayani Pangani katika mwaka huu wa fedha 2024/2025.
Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa wilaya ya Pangani Gift Msuya wakati akizungumza na Pangani FM Ofisini kwake leo huku akivitaja vitongoji vitakavyonufaika na mradi huo.
Amesema mpaka sasa Wilaya ya Pangani imefikiwa na huduma ya umeme katika vitongoji 60 kati ya vitongoji 96.
Huu ni mwendelezo wa utekelezaji wa miradi ya umeme wilayani Pangani ambapo mwaka wa fedha 2023/24 wilaya hiyo ilipokea shilingi bilioni nne kwa ajili ya kusambaza umeme vijiji.