Dkt. Biteko awataka wazazi, walimu kutengeneza mazingira salama ya mtoto
11 October 2024, 2:43 pm
“Samia wa kesho anajengwa na mzazi, mwalimu na mwanafunzi mwenyewe hivyo tuache tabia ya kutumia lugha ambazo zitawakatisha tamaa watoto wetu kuifikia kesho yenye mafanikio” Dokta Biteko
Na Kokutona Banyikila
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dokta Dotto Biteko amewataka wazazi na walimu kushirikiana katika kutengeneza mazingira salama ya mtoto leo
Ameitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mtoto wa leo Samia wa Kesho iliyofanyika katika wilaya ya Muheza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya juma la elimu katika wilaya hiyo
Pia ametoa wito kwa wazazi kuacha kutumia lugha zisizo na staha kwa Watoto wao na kuwalea katika maadili
Kampeni hiyo ya miaka mitano inawashirikisha wadau wa Sekta ya Elimu katika Wilaya ya Muheza mkoani Tanga kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo