Pangani FM

Ulinzi wa misitu Pangani, wananchi kupata fursa mpya ya ajira

8 September 2024, 1:54 pm

Baadhi ya wajumbe wa kamati ya mazingira kijiji cha Mkwaja wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya ugawaji wa majiko banifu.

Tangu shirika la UZIKWASA lilipoanza kutoa elimu ya utengenezaji wa majiko banifu jamii imeonesha uhitaji mkubwa wa majiko hayo kutokana na kutumia kuni chache hivyo kuanzisha fursa mpya ya ujira kwa wanajamii wilayani Pangani.

Na Cosmas Clement

Wajumbe wa kamati ya mazingira kijiji cha Mkwaja wilayani Pangani wameshukuru shirika la UZIKWASA kuwapelekea Mradi wa mazingira kwani umewawezesha kuibua shughuli mbadala za kupata kipato.

Shughuli hizo mbadala za kuwaingizia kipato zinakuja baada ya shughuli zao za awali za uvuvi na uchuuzi wa samaki kuathiriwa na mabadiliko ya tabia Nchini.

Wakizungumza wakati wa mafunzo saidizi yaliyoenda sambamba na utoaji wa majiko banifu, wajumbe hao wamesema mafunzo waliyoyapata chini yamradi huo yamewawezesha kubuni miradi ya kilimo cha bustani, na ufugaji.

sauti ya wajumbe mkwaja

Pia wamesema mradi wa utengenezaji wa majiko banifu unawapa fursa ya ajira kwa kuongeza kipato kutokana na kuongezeka kwa uhitaji .

Sauti ya wajumbe wa kamati ya mkwaja

Kwa upande wake bwana Nickson Lutenda mwezeshaji kutoka UZIKWASA amesema mradi huo wa majaribio utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

Sauti ya bwana Nickson Lutenda