Jinsi mikoko inavyotumiwa na wageni kuwa sehemu ya haja katika kijiji cha Kipumbwi
2 September 2024, 6:30 pm
Kijiji cha Kipumbwi miongoni mwa vijiji vinavyoongoza kwa ukusanyaji wa mapato katika halmashauri ya wilaya ya Pangani, ina choo kimoja cha wageni chenye matundu 11.
Na Cosmas Clement
Wananchi wa Kijiji cha Kipumbwi wilayani Pangani wameiomba serikali kujenga vyoo kwa ajili ya kuwahudumia maelfu ya wageni wanaofika kijijini hapo kwa ajili ya shughuli za uvuvi.
Wakizungumza na Pangani FM wakazi hao wamesema kwa sasa wageni hutumia choo kimoja cha mtu binafsi chenye matundu kumi na moja ambayo ni wanaume ni 7 na wanawake 4 ambayo wamedai hayatolezi umati huo wa watu hivyo kuhatarisha jamii na magonjwa ya mlipuko
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kipumbwi Bwana Ally Bahorera pamoja na kukiri uwepo wa changamoto hiyo, amesema serikali ya Kijiji imeshalifikisha suala hilo katika ofisi ya halmashauri ya wilaya ya Pangani ili kupata mkandarasi.
Kijiji cha kipumbwi kilichopo katika ukanda wa mwambao wa Bahari ya hindi hupokea idadi ya wageni zaidi elfu mbili kila bamvua la uvuvi hivyo kutokana na changamoto ya uhaba wa vyoo hupelekea wengi wao kujisaidia kwenye fukwe na kwenye mikoko.