Pangani FM

Jinsi bodaboda walivyobadili mtazamo wa jamii wilayani Pangani

29 August 2024, 12:27 pm

Baadhi ya vijana wa bodaboda wakifuatilia mada wakati wa mafunzo yanayotolewa na shirika la Uzima Kwa Sanaa (UZIKWASA) katika ofisi za shirika hilo zilizopo kijiji cha Boza wilayani Pangani.

Shirika la Uzima Kwa Sanaa (UZIKWASA) limekuwa likiwezesha kundi hilo la bodaboda wilayani Pangani hivyo kuwezesha kubadili tabia za vijana hao ambao awali baadhi yao walikuwa wakihusishwa na vitendo vya ukatili kwa wasichana.

Na Majabu Ally

Bodaboda wilayani Pangani mkoani Tanga wameaswa kuwa chachu ya mabadiliko katika kudhibiti vitendo vya kikatili visijitokeze katika jamii zao.

Hayo yamejiri katika nyakati ambazo vitendo vya kikatili vikitajwa kushamiri katika maeneo mbalimbali hapa nchini  huku serikali na wadau wakitafuta mbinu za kutokomeza vitendo hivyo.

Shirika la UZIKWASA lililopo wilayani Pangani ni miongoni mwa wadau wanaotoa mafunzo ya uongozi wa mguso na mafunzo ya kukabiliana na ukatili kwa makundi mbalimbali yaliyopo katika jamii.

Taarifa kamili na mwandishi wetu Majabu Madiwa aliyeshiriki katika siku ya kwanza ya mafunzo hayo

Mafunzo yaliyoanza jana Jumatano yanaendelea kwa siku mbili zaidi hadi siku ya Ijumaa