Pangani FM

Wazazi Pangani waaswa kuhudhuria vikao vya shule

5 August 2024, 6:32 pm

Walimu walezi wilayani Pangani wakiwa kwenye Picha ya pamoja katika ofisi za shirika la UZIKWASA baada ya mafunzo ya Uongozi wa Mguso

Shirika la Uzima kwa Sanaa ( UZIKWASA) Limekuwa na utaratibu wa kutoa mafunzo kwa walimu ili kuwajengea uwezo wa kuwalinda wananfunzi dhidi ya ukatili wa kijinsia.

Na Saa Zumo

Wazazi kutoudhuria vikao vya shule kunatajwa kukwamisha maendeleo ya taaluma kwa wanafunzi wa shule za sekondari wilayani Pangani mkoani Tanga

Hayo yamejiri katika mafunzo ya Uongozi wa mguso yanayotolewa na shirika la Uzikwasa yakiwa na lengo la kuwawezesha na kutoa mbinu kwa walimu walezi wa shule za sekondari kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa vinavyowakabili wanafunzi.

Muwezeshaji kutoka shirika la uzikwasa ndugu Eric Malya amesema kikao hicho kimesaidia kujuwa masuala mbali mbali ni uwepo wa changamoto ya wazazi kutokuweka msisitizo wa mienendo ya kitabia kwa watoto wao.

Sauti ya bwana Eric Malya mwezeshaji kutoka UZIKWASA

Pia ametaja lengo la mafunzo hayo na kusema yatasaidia kuwapa mkao mpya utakao Saidia kuwapa mbinu zitakazo wasaidia katika majukumu yao.

Sauti ya bwana Eric Malya mwezeshaji kutoka UZIKWASA

Baadhi ya washiriki wameelezea namna mafunzo hayo watakavyo yatumia ikiwemo kusikiliza jambo kwa kila hatua ili kuweza kulitatua.

Sauti ya washiriki wa mafunzo hayo

Mafunzo hayo yaliwashirikisha walimu wa shule za sekondari kwa upande wa serikali na binafsi wilayani Pangani na yalichukuwa siku tatu kuwanoa kwa kuwapa muelekeo mpya wa kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.