Ukusanyaji mapato mazao ya misitu ya vijiji yawaibua madiwani Pangani
2 August 2024, 9:58 pm
Wakala wa Huduma za Misitu umeundwa kwa madhumuni ya kuhakikisha; Uwepo wa usimamizi madhubuti na wenye ufanisi na tija wa rasilimali za misitu na nyuki, kuongeza ubora na thamani ya kifedha katika kutoa huduma kwa umma; na kuendelea kukuza na kuboresha uwezo wa kutoa huduma kwa umma.
Na Cosmas Clement
Hatua hiyo imetokana na hoja iliyoibuliwa na Diwani wa kata ya mikinguni Mheshimiwa Joel Mrutu, katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika julai 31 mwaka huu katika ukumbi wa halmashauri ya zamani ya wilaya ya Pangani.
Katika hoja yake Mheshimiwa Joel alieleza kuwa kuna baadhi ya vijiji vinaendesha shughuli za uvunaji wa msitu wake wa asili lakini hawahusiki kukusanya ushuru wa mazao ya msitu huo.
Kwa upande wake Meneja Muhifadhi TFS Bwana Eliapenda Wavii ameelezea jinsi TFS inavyowajibika katika ukusanyaji wa mapato ya mazao ya misitu.