Zingatia haya kuimarisha afya yako
25 July 2024, 3:28 pm
Siku ya Afya na Lishe inapaswa kufanyika kwa kila kijiji mara nne kwa mwaka kwa vipindi vya miezi mitatu ili kutoa elimu kwa jamii juu ya milo sahihi.
Na Cosmas Clement
Wananchi katika kijiji cha Pangani Mashariki wametakiwa kuzingatia lishe bora ili kupunguza changamoto za kutozingatia lishe ikiwemo upungufu wa damu kwa wakinamama wajawazito.
Hayo yameelezwa na Afisa lishe wilaya ya Pangani Bwana Daudi Mwakabanje ambapo ametanabaisha uwepo wa tatizo la udumavu kwa watoto na upungufu wa damu kwa wanawake kipindi cha ujauzito.
Kwa upande wake Mtendaji kata ya Pangani Mashariki Bwana Mponji Kaziyabwana amesema Kata hiyo imesaini Mkataba na ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri ya Pangani juu ya utekelezaji wa afua za lishe.
Nao wakazi wa kijiji hicho waliohudhuria maadhimisho hayo wameelezea kupata elimu ya lishe bora itakayowawezesha kufuata milo sahihi katika familia zao.
Maadhimisho ya siku ya afya na lishe ngazi ya kijiji hufanyika kila baada ya miezi mitatu kwa mwaka. Ambapo kijiji cha Pangani Mashariki hapo jana kimeadhimisha siku ya afya na lishe.