Vijana Pangani wakataa uvivu, wajitosa bandarini
25 July 2024, 2:32 pm
Bandari ya mji wa Pangani imeajiri zaidi ya vijana 200 kwa kujihusisha na shughuli za kubeba mizigo.
Wakizungumza na Pangani FM baadhi ya vijana wanaojihusisha na ubebaji wa mizigo bandarini hapo wamesema shughuli hizo zimeimarisha hali ya vipato vyao.
Bwana Riziki Nyoro ambaye ni mwenyekiti wa kikundi cha wapakia mizigo bandarini hapo, amesema mpaka sasa wamewapokea vijana 250 ikionyesha uwepo wa vijana wengi wa Pangani wanaopenda kujishughulisha tofauti na ilivyozoeleka.
Aidha wameeleza jinsi wanavyozingatia usalama wakati wa kuendesha shughuli ushushaji na upakiaji wa mizigo.
Bandari ya mji wa Pangani kwa sasa inahudumia shughuli za usafirishaji wa mizigo kwenda na kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.