Pangani FM

Shilingi milioni 600 kujenga shule ya Ufundi Pangani

27 June 2024, 9:37 pm

Mkuu wa wilaya ya Pangani Mussa Kilakala akizungumza katika mkutano wa chama kuwasilisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi 2020/2025.

Ujenzi wa shule ya ufundi unatarajiwa kuleta hamasa kwa wanafunzi wa Pangani kujifunza masomo ya sayansi.

Na Hamisi Makungu

Shule Mpya ya Sekondari ya UFUNDI itakayogharimu kiasi cha Shilingi Milioni 600 inatarajiwa kujengwa Wilayani Pangani katika Mwaka wa Fedha 2024/2025.

Ameyasema hayo Mkuu wa Wilaya ya Pangani wakati akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa IIani ya Chama cha Mapinduzi CCM Pangani kwa kipindi cha miezi Sita.

Aidha amesema Shule hiyo inatarajiwa kutimiza ndoto za watoto wa Wilaya ya Pangani kwa kuwaongezea maarifa na ujuzi ili waweze kujitegemea kwa kujiajiri au kuajiriwa.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Pangani Bwana Mussa Kilakala

DC Kilakala ameongeza kuwa Serikali imeendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kujenga na kukarabati Miundombinu ya Shule, ili kufanikisha haki ya kupata elimu bora kwa watoto wa Wilaya ya Pangani.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Pangani Bwana Mussa Kilakala