Pangani FM

Majiko banifu yatolewe kwa familia duni

3 June 2024, 10:00 am

Wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA na Mazingira wakiwa kwenye mchakato wa kuandaa majiko banifu katika mafunzo yanayotolewa na shirika la Uzima kwa Sanaa.

Majiko banifu itawasaidia familia duni kuchangia katika mapambano ya mabadiliko ya tabia nchi kwakuwa uwezo wao ni mdogo katika kumudu gharama za aina nyingine za nishati safi ya kupikia.

Na Abdilhalim Shukuran

Kamati ya MTAKUWWA na mazingira katika Kijiji cha Mbulizaga zimeshauriwa kugawa majiko banifu kwenye kaya zenye hali duni kijijini hapo ili kwa pamoja washiriki katika kuchukua hatua za kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabia nchi.

Akizungumza na kamati hizo Katika Kijiji cha MBULIZAGA Wilayani Pangani Mkoani Tanga mwezeshaji kutoka shirika la Uzima kwa Sanaa (UZIKWASA) NICKSON LUTENDA amezitaka kamati hizo kipaumbele Kaya ambazo hazijimudu kiuchumi wakati wa zoezi hilo.

Sauti ya Bwana Nickson Lutenda mwezeshaji kutoka shirika la UZIKWASA

Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wamelipongeza shirika la UZIKWASA kwa uwezeshwaji wa vifaa vitakavyo wawezesha kutengeneza majiko banifu yanayosaidia kupunguza matumizi ya kuni.

Sauti za wajumbe wa kamati ya mazingira na MTAKUWWA ya kijiji cha Mbulizaga.

Shirika la UZIKWASA linaendelea na zoezi la kutoa mafunzo katika vijiji vya wilaya ya Pangani katika afua mbalimbali ikiwemo utunzaji wa mazingira.