Muheza wajadili, mikakati kuboresha elimu
31 May 2024, 11:07 pm
Ili kufanikiwa katika kuboresha elimu inatuhitaji kuwa na nguvu ya pamoja na mikakati ya kutuvusha hapa tulipo.
Na Hamisi Makungu
Serikali ya Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga imefanya kikao kazi chenye lengo la kuongeza ufanisi wa wilaya hiyo katika sekta ya elimu.
Akiongea katika kikao hicho mkuu wa wilaya hiyo BI ZAINAB ABDALLAH ISSA amekitaka kikao hicho kitoke na mkakati ambao utawezesha wilaya hiyo kushika nafasi za juu katika sekta ya elimu
Baadhi ya washiriki wa kikao hicho akiwemo Afisa elimu sekondari Selepion Bashange na Afisa elimu awali na msingi Pili Maxmilian wameeleza hali ilivyo katika shule hizo na mkakati wa kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri katika masomo yao.
Wilaya hiyo imeweka mkakati wa kuhakikisha wanafunzi wanasoma katika mazingira rafiki na walimu wanapata hali ya kufundisha kwa kuboresha mazingira ya kufundisha na kufundishia.