Miaka 60 ya Muungano, Pangani yajivunia miradi ya kimkakati
27 April 2024, 2:21 pm
Mafanikio ya miradi ya kimkakati miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanafaa kujivunia.
Na Hamisi Makungu
Wananchi wa Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga wametakiwa kuisherehekea Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kujivunia Mafanikio na Miradi ya Kimkakati inayoendelea kutekelezwa Wilayani humo.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Musa Kilakala kwenye salamu zake wakati akizungumza katika hafla fupi ya kubariki Jengo Jipya la Kituo cha Radio Pangani lililopo Kijiji cha BOZA Kata ya Kimang’a.
Sambamba na hilo amewaomba Viongozi wa Dini kuendelea kuliombea Taifa, Mheshimiwa Rais na wasaidizi wake ili waendelee kupigania maendeleo ya watanzania.
Katika hatua nyingine amesema wilaya ya Pangani inatarajiwa kutoa fursa ya ajira kutokana na mradi wa uchimbaji wa madini yaliyoonekana kufutia utafiti uliyofanywa katika maeneo mbalimbali ya ukanda wa Pwani wilayani humo.