Pangani FM
Tozo za miamala kujenga Kituo cha Afya cha Madanga.
16 November 2021, 1:34 pm
Halmashauri ya Wilaya ya Pangani imepokea kiasi cha fedha Shilingi Milioni 250 kutoka katika mgao wa fedha zotokanazo na tozo za miamala ya simu.
Akizungumza na Pangani FM Mkurugenzi wa Hlamshauri ya Wilaya ya Pangani Bw. Isaya Mbenje amesema kuwa fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa Kituo cha Afya cha Tarafa ya Madanga.