Sengerema FM
Sengerema FM
30 October 2026, 7:07 am

Dawa za filic Acid ni mhimu kwa mama mjamzito kwasababu husaidia kuongeza damu mwilini,kumkinga mtoto na kuzaliwa mwenye changamoto ya kichwa kikubwa au mgongo wazi.
Na;Emmanuel Twimanye
Wanawake wajawazito Wilayani Sengerema wametakiwa kuacha tabia ya kutotumia vidonge vya kuongeza damu kwa madai kuwa vinaongeza siku za kujifungua .
Akizungumza kwa niaba ya Mganga mkuu wa wilaya ya Sengerema Bi, Recho Ntogwisangu wakati akitoa elimu ya uzazi kwa wananchi amesema kuwa baadhi ya wanawake wajawazito hawatumii vidonge hivyo ili hali vianasaidia kuongeza damu na kutopata mtoto mlemavu mwenye kichwa kikubwa au mgongo wazi .
Kwa upande wao ,baadhi ya wanawake wajawazito wamkiri kutotumia vidonge hivyo kwa madai ya kuongeza siku za kujifungua huku wakiahidi kuzitumia baada ya kupata elimu hiyo.