Sengerema FM

DC Sengerema aongoza wananchi kupanda miti miaka 60 ya muungano

24 April 2024, 8:00 pm

Mkuu wa wilaya ya Sengerema Bi. Senyi Ngaga na baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye zoezi la kupanda miti kama kumbukumbu ya miaka 60 ya muungano.Picha na Piter Marlesa

Katika Zoezi hili la Kumbukizi ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar jumla ya miche 800 imepandwa katika eneo la Hospitali ya Wilaya ya Sengerema sambamba na kufanya usafi katika Eneo hilo.

Na:Kelvin Philipo

Wananchi Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wametakiwa kuendelea kutunza mazingira ikiwa ni pamoja na upandaji miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Baadhi ya Viongozi kutoka wilaya ya Sengerema wakiongozwa na Mhifadhi TFS Bwn.James Aloyce wakiwa kwenye picha ya Pamoja.Picha na Piter Marlesa

Wito huo umetolewa leo na mkuu wa wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga wakati akiongoza zoezi la upandaji miti katika Hospitali ya Wilaya iliyopo katika kata ya Mwabaluhi ambapo miti Zaidi ya mia nane imepandwa kwa kushirikiana na viongozi pamoja na wadau mbalimbali wa mazingira.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga

Naye mhifadhi wa huduma za misitu Tanzania Wilayani Sengerema James Aloyce amesema suala la upandaji miti ni endelevu ilikulinda na kuhifadhi mazingira huku  wakitarajia kufikisha MICHE laki mbili ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Sauti ya Mhifadhi wa huduma za misitu Tanzania Wilayani Sengerema Bwn. James Aloyce

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema Wilbard Bangora amesema watahakikisha miti hiyo inatunzwa kwa uangalifu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Sauti ya Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema Wilbard Bangora

Hata hivyo zoezi la upandaji miti linafanyika nchini kote kuelekea kilele cha maadhimisho ya Sikukuu ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika April 26 mwaka huu.