Sengerema FM

Wanusurika kifo baada ya kula samaki wanaodaiwa kuwa na sumu Sengerema

8 February 2024, 7:23 pm

Manusura wa tukio walio kula samaki anaye daiwa kuwa na Sumu. Picha na Said Mahera

Matukio ya watu kula samaki wanaodaiwa kuwa na sumu hutokea kwa baadhi ya maeneo hapa nchini ambapo katika kijiji cha Igaka ndio mara ya kwanza kutokea.

Na:Said Mahera

Watu saba wa familia moja wamenusulika kifo baada ya kula mbonga aina ya samaki inayosadikiwa kuwa na sumu katika kitongoji cha Igaka Senta Wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Wakisimulia  tukio  hilo baadhi  ya wanafamilia walionusulika kufa baada ya kutumia samaki hiyo wamesema baada ya kula   gafra wakaanza kuumwa tumbo na kupelekwa  katika  zahanati iliyopo  kijijini  hapo.

Sauti ya Manusula wa wa tukio walio kula samaki

Naye  baba wa familia   iliyonusulika Ndg Edson Simba amesema  baada  ya  kununua  samaki  yule  na  kumpeleka  nyumbani  kwa  ajili  ya  maandalizi  ya  kutumika  usiku,  yeye  alitoka na  kuelekea  sengerema,ndipo  alipopigiwa  simu na  kupewa  taarifa ya  familia  yake  kuuguwa  baada  ya  kula  samaki  huyo.

Sauti ya baba wa familia walio nusulika Ndg Edson Simba

Kwa upande wao majirani  akiwemo mchungaji wa kanisa la  AICT igaka  wamesikitishwa na tukio hilo huku wakilani tukio hilo la kushangaza huku mchungaji akiwaomba watu kuwa na hofu ya mungu.

Sauti ya majirani wa Familia hiyo

Hata hivyo  muhudumu wa afya ngazi ya jamii ndg Magambo Kengele    amesema baada ya kuwapokea wagonjwa hao amewapa huduma ya kwanza kwa kuwanywesha maziwa na baadae kuwapeleka hospitalini kwa  matibabu  zaidi.

Sauti ya muhudumu wa afya ngazi ya jamii ndg Magambo Kengele 

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mwenyekiti wa kitongoji cha igaka senta Bwn Emanuel Thobias  amesema watu hao kutoka familia moja baada ya kula samaki matumbo yalianza kuuma na kukosa nguvu na kupelekwa katika  hospitali.

Sauti ya mwenyekiti wa kitongoji cha igaka senta Bwn Emanuel Thobias