Sengerema FM

Amuua mke kisa wivu wa kimapenzi

16 April 2024, 4:00 pm

Baadhi ya majirani waliofika kwenye tukio la mwanamme kumu ua mke wake.Picha na Said Mahera

Matukio ya kujeruhi na kuua wenza wao yamezidi kushamili katika maeneo ya Kanda ya ziwa hasa katika wilaya ya Sengerema ambapo zaidi ya matukio matano yameripotiwa kutokea ndani ya miezi mitatu.

Na:Said Mahera

Mwanamme mmoja aliyejulikana kwa jina la Jackson kalamji Sahani [50] mkazi wa Kitongoji cha Isegeng’he kijiji cha Mwamanyili kata ya Bukokwa Halimashauri ya Buchosa Wilayani Sengerema anadaiwa kumuua mke wake kwa  kumchoma na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali ya mwili wake kwa madai ya wivu wa kimapenzi.

Baadhi ya majirani wa familia wamesikitishwa na kitendo hicho na kuiomba serikali kumchukulia hatua kali mwanaumme huyo aliyedaiwa kufanya   tukio hilo la kinyama ili kukomesha matukio ya mauwaji.

Sauti za wananchi na majirani

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mwenyekiti wa kitongoji cha Isegenye Bwn  Joackimu Nyelembi amemtaja mwanamke aliyeuwawa kuwa ni   Mariamu Charles [42]   huku mwenyekiti wa kijiji  cha Mwamanyili Bwn Dominiko Kashonele amesema  mwanaume huyo baada ya kutekeleza mauwaji hayo amejisalimisha kituo cha polisi cha Nyakalilo.

Sauti za viongozi wa Serkali ya kijiji cha Isegenye

Hata hivyo Diwani wa kata ya Bukokwa Mh Yusufu Busumba  amelaani tukio hilo na kuwaomba wananchi kuwa watulivyu wakati serikali ikifanya uchunguzi dhidi ya tukio hilo.

Sauti ya Diwani wa kata ya Bukokwa Mh Yusufu Busumba

Hata hivyo jeshi la polisi Wilaya ya Sengerema limefika katika eneo la tukio na kuruhusu shughuli za mazishi kuendelee huku wakiwataka wananchi kutojihusisha na matukio ya kihalifu pamoja na  kutojihusisha na madawa ya kulevya ikiwemo uvutaji wa bangi.