Sengerema FM
Sengerema FM
6 May 2026, 9:27 am

Katika maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani May mosi 2026 afsa tarafa wa Nyanchenche wilayani Sengerema ameibuka mfanya kazi hodari kutoka ofsi ya mkuu wa wilaya ya Sengerema, ambapo wananchi wa eneo hilo wamempongeza kwa uchapa kazi wake.
Na;Said Mahera
Afisa Tarafa wa Nyanchenche wilayani Sengerema, Bi. Happynes Juma amewashukuru wananchi wa taarafa hiyo kwa ushirikiano wanaouonesha katika shughuli za maendeleo.
Akizungumza baadaya kupokea cheti cha mfanyakazi hodari wa umma Bi. Happynes Juma amesema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano mzuri anaoupata kutoka kwa viongozi wenzake pamoja na wananchi kwa ujumla, nakueleza kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo, ikiwemo sekta ya elimu.
Aidha, Bi.Happynes Juma amebainisha kuwa mbali na mafanikio katika elimu, ameweza pia kushughulikia na kupunguza kwa kiasi kikubwa migogoro ya ardhi katika eneo hilo.
Kwa upande wao wananchi wa Tarafa ya Nyancheche wamempongeza kwa kutunukiwa cheti hicho na kusema amekuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha shunguli zamaendeleo zinastawi.
Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Buyagu Ezekieli Eliyud Kisanga amempongeza Afisa Tarafa huyo kwa kupata tuzo hiyo, akiahidi kuendelea kumpa ushirikiano katika kusukuma mbele shughuli za maendeleo kwa manufaa ya wananchi.
Tarafa ya Nyacheche iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema inajumuisha kata nne ambazo ni Igalula, Kagunga, Buyangu na Bitoto.