Sengerema FM

Mtoto afariki kwa kushambuliwa na Fisi

5 July 2023, 1:54 pm

Fisi anayesadikiwa kujeruhi. Picha kwa msaada wa mtandao

Kutokana na kuongezeka kwa matukio ya Fisi kushambulia watu na mifungo wilayani sengerema, hali hiyo imezua hofu, huku baadhi yao wakishindwa kufanya shughuli za maendeleo

Na:Emmanuel Twimanye

Mtoto   mwenye umri wa  miaka 5  aliyeshambuliwa na Fisi na kujeruhiwa sehemu  mbalimbali za  mwili  wake    katika Kitongoji cha chamigumo  Kijiji  cha  Nyantakubwa Kata ya Kaungamile Wilayani Senggerema Mkoani Mwanza  amefariki Dunia.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha chamigumo Elias Malika amethibitisha  mtoto  mathias  Enock  kufariki Dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza.

Baadhi ya wananachi wa Kitongoji hicho  licha ya kusikitishwa na tukio hilo  wametumia  msiba huo  kuiomba serikali kukabiliana na fisi hao ili kunusuru maisha ya wakazi wa eneo hilo kwa kuwa kwa sasa wanaishi kwa hofu kubwa.

Sauti ya mwandishi wetu Emmanueli Twimanye akiripoti taarifa kutokea kijiji cha Nyantakubwa