Sengerema FM

Wananchi watakiwa kuchukua tahadhali ya kipindupindu

10 January 2024, 6:25 pm

Wataalamu wa Afya kutoka ofsi ya mganga mkuu wa wilaya ya Sengerema wakizungumzia changamoto ya ugonjwa wa Kipindupindu,wakwanza Bwn. Abdul Mgonja na wa pili Bwn. Charles Manyanga. Picha na Piter Marlesa

Changamoto ya kipindupindu imetajwa kuenea kwa kasi zaidi hasa kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa ikianzia katika wilaya ya Bariadi mkoa wa Simiyu, ambapo mpaka sasa katika mkoa wa Mwanza wamebainika wagonjwa wa kipindupindu 27 kwenye maeneo ya wilaya ya Magu na Mwanza jiji.

Na:Emmanuel Twimanye.

Wananachi Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wametahadharishwa kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Kipindupindu hususani  katika kipindi hiki cha mvua zinazoendelea kunyesha.

Tahadhari hiyo imetolewa na mtaalamu kutoka ofisi ya Mganga mkuu wa Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Charles Manyanga  kufuatia ugonjwa huo kutokea katika  Halamshauri ya Nyamagana na Ilemela Mkoani Mwanza.   

Katika hatua nyingine mtaalamu huyo  ameitaka  jamii kutoficha  taarifa za wagonjwa  badala yake watoe taarifa kwa  afisa mtendaji wa kijiji ama wa kata ili  wagonjwa wapelekwe haraka kwenye  kituo cha kutolea huduma kwa ajili ya kupatiwa  tiba stahiki.

Nao baadhi ya wananchi wilayani humo wameahidi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo .

Taarifa ya Emmanuel Twimanye inafafanua zaidi.