Sengerema FM

Utumiaji wa ugoro chanzo kansa ya mdomo kwa vijana

23 April 2024, 7:57 pm

Mganga mkuu mkoa wa Geita Dr.Omar Sukari akizungumza.Picha na Emmanuel Twimanye

Kufatia kuwepo na wimbi kubwa la vijana nchini kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya ikiwemo ugoro, jamii imeonywa kuachana na matumizi ya madawa hayo ili kuondokana na madhara yanayoweza kumpata ikiwemo kupata kansa.

Na:Emmanuel Twimanye

Vijana   Wilayani  Sengerema  Mkoani Mwanza  wametakiwa   kuachana na matumizi ya ugoro ili kuepuka kukumbwa na  magonjwa  mbalimbali  ikiwemo kansa ya mdomo.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita Dkt Omary Sukari  wakati akizungumza na radio Sengerema , kufuatia  kuwepo kwa wimbi kubwa la vijana wanaojihusisha na matumizi ya ugoro.

Amebainisha kuwa  ugoro una madhara makubwa ikiwemo  kusababisha  magonjwa mbalimbali  kama  kansa ya  mdomo,   koo na kongosho hivyo ni vyema vijana  wakaachana na  matumizi hayo ya ugoro.

Sauti ya Mganga mkuu wa mkoa wa Geita dr. Omar Sukari

Naye mmoja kati ya wauzaji wa ugoro  Wilayani  Sengerema  amesema kuwa pamoja na kuyauzia makundi mengine  bidhaa hiyo lakini  wateja wake wakuu  kwa sasa ni vijana wa kike na kiume.  

Sauti ya muuzaji wa ugoro mjini Sengerema

Nao baadhi ya wananchi  wameshangazwa na kitendo cha baadhi ya vijana katika kipindi hiki  kutumia ugoro kwa kuwa  jambo hilo lilikiwa limezoeleka  kwa    wazee.

Sauti za baadhi ya wananchi wakazi wa mji wa Sengerema

Kwa uapande wao baadhi ya vijana wanaotumia ugoro walipotafutwa na Radio Sengerema kwa ajaili ya kuzungumzia suala hilo hawakutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari.

Aidha  kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani WHO zinaonyesha utumiaji wa bidhaa za Tumbaku husababisha vifo kwa karibu nusu ya watumiaji wake na zaidi ya watu takribani Milioni 8 hufariki kila mwaka kutokana na matumizi ya Tumbaku.