Sengerema FM

TUCTA Mwanza waitaka serkali kuchukua hatua kwa waajiri wanao nyanyasa wafanyakazi.

2 May 2023, 11:40 am

Picha: Katibu TUCTA Mwanza akikabidhi cheti cha pongezi ofisi ya mkuu wa mkoa kwa katibu tawala mkoa wa Mwanza

Chama cha wafanyakazi Mkoani Mwanza  TUCTA kimelaani vikali  waajiri wanaowanyanyasa wafanyakazi  sehemu za kazi ikiwemo kutowalipa stahiki zao kwa wakati.

Hayo yamesemwa na katibu wa chama cha wafanyakazi mkoani mwanza Zebedayo Athuman wakati akisoma risala kwa mgeni rasmi katika  maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani,ambapo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya mnadani Wilayani Sengerema.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Adam Malima amewahakikishia watumishi wa kada mbalimbali  kuwa atashughulikia changamoto zote zinazowakabili ili waweze kufanya kazi katika mazingira rafiki .

Hata hivyo baadhi ya watumishi wa kada mbalimbali waliopatiwa tuzo za ufanya kazi bora wameahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuchochea maendeleo ya taifa .

Taarifa ya Mwandishi wetu Anna Elias inafafanua zaidi.