Sengerema FM

Wazazi watakiwa kufuatilia mienendo na malezi ya watoto wao

31 October 2023, 8:55 pm

Mratibu wa dawati la jinsia na watoto jeshi la polisi wilayani Sengerema Afande Mponela Malongo akitoa elimu ya ukatili kwa watoto. Picha Emmanuel Twimanye

Wazazi na walezi wilayani Sengerema mkoani Mwanza wanatajwa kujali zaidi shughuri zao binafsi na kuonyesha kulitegea mgongo suala la malezi kwa watoto, huku wenginge wakiwaachia watoto kuwalea watoto wenzao.

Na:Emmanuel Twimanye.

Wazazi Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza  wametakiwa   kutimiza jukumu la malezi ya watoto badala ya kuwacha watoto  wajilee wenyewe  hali inayohatarisha usalama wa maisha yao.

Kauli hiyo imetolewa na Mratibu wa Dawati la Jinsia na watoto kutoka jeshi la polis Wilayani Sengerema Mponela Malongo  kufuatia baadhi ya wazazi kushindwa kutimiza jukumu la malezi kwa watoto na kusema kuwa jukumu la kulea watoto ni la mzazi na si mtoto.

Katika hatua nyingine ameiomba jamii  kuacha kuficha matukio ya ukatili  pindi wanapofanyiwa watoto  kwa madai ya kulipwa fedha na wahusika  kwa kuwa  hali hiyo inamwathiri mtoto.

Nao baadhi ya wazazi  wamekiri kutotekeleza suala la malezi kwa watoto kwa madai ya kujikita katika shughuli za kutafuta kipato cha familia.

Taarifa ya Emmanuel Twimanye Inafafanua zaidi