Sengerema FM

Kijana ajitosa kwenye maji kutoka kwenye kivuko Ziwa Victoria

9 February 2024, 8:02 pm

Kivuko cha Mv.Kome II kikiwa kinaendelea na safari zake za kusafirisha abilia kutoka Nyakaliro na Kisiwa cha Kome Sengerema. Picha na wizara ya uchukuzi

Matukio ya Watu kujitosa kwenye maji yameanza kujitokeza ambapo mwanzoni mwa mwaka huu kijana mmoja alijitosa baharini kutoka katika boti ya Zanzibar III na mwili wake ukapatikana baada ya siku 3.

Na.Said Mahera

Kijana mmoja aliyejulikana kwa majina ya Mashauri  Masanja 23 amejirusha majini kutoka kwenye Kivuko cha Mv.Kome II Kinachofanya safari zake kati ya Nyakarilo na kisiwa cha Kome kilichopo Halmashauri ya Buchosa.

Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa serkali ya kijiji cha Nyakarilo Ndg. Silvester Kabinga Mgema amesema kivuko hicho kilikuwa ndo kimeanza kuondoka umbali wa km. moja na nusu kutokea Nyakalilo kuelekea  Kome.

Kivuko cha Mv Kome II kinatani 50, kina uwezeo wa kubeba abiria 120, magari makubwa matatu na madogo sita lakini kinabeba zaidi kutokana na wingi wa abiria  kisiwa cha Kome.

Tukio hilo limetokea Feb 08 majira ya saa tisa na nusu ambapo mwenyekiti huyo amewataka ndugu na jamaa kufika eneo la Nyakarilo ili kusaidia shughuli za utaftaji.

Mahojiano ya Mwandishi wetu Said Mahera na Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyakarilo Ndg.Silvester Kabinga Mgema