Sengerema FM

Mitishamba chanzo cha vifo vitokanavyo na uzazi Sengerema

14 March 2024, 3:51 pm

Bi.Marry Mgoa mratibu wa afya ya mama na mtoto Halmashauri ya Sengerema.Picha na Piter Marlesa

Vifo vitokanavyo na uzazi wilayani Sengerema vimekuwa vikitajwa kuongezeka kutokana na mwitikio mdogo wa akinamama wajawazito kuhudhuria kliniki kwa wakati na matumizi ya dawa za kienyeji.

Na:Elisha Magege

Matumizi ya dawa za kienyeji yatajwa kuwa chanzo cha vifo vya akinamama wajawazito katika halmashauri ya Sengerema mkoani mwanza.

Hayo yameelezwa na Bi.Marry Mgoa mratibu wa afya ya mama na mtoto Halmashauri ya Sengerema kwenye kipindi cha safari mseto kinachorushwa na Radio Sengerema, ambapo amesema takwimu zinaonyesha ni asilimia 37 pekee ya akinamama waliohudhulia kiliniki kwa kipindi cha kuanzia mwezi January mwaka huu 2024.

Sauti ya Bi.Marry Mgoa mratibu wa afya ya mama na mtoto Halmashauri ya Sengerema

Katika hatua nyingine amesema mama mjamzito anapowahi kituo cha kutolea huduma za afya akiwa na mwenzi wake hupewa ushauri na vipimo vya magonjwa mbalimbali yanayoweza kumdhuru mtoto akiwa tumboni.

Sauti ya Bi.Marry Mgoa mratibu wa afya ya mama na mtoto Halmashauri ya Sengerema

Hata hivyo Halmashauri ya Sengerema imetajwa kuwa ya pili katika mkoa wa Mwanza kwa vifo vya akinamama wajawazito ikitanguliwa na halmashauri ya Nyamagana.