Sengerema FM

Amuua kwa madai ya kugoma kurudiana nae

7 March 2024, 10:33 pm

Baadhi ya Ndugu na majirani waliofika nyumbani kwa marehemu Vumilia mshimo. Picha na Emmanuel Twimanye

Matukio ya wanadoa kutarakiana wakiwa wanapendana yamekuwa chanzo cha mauaji kwa wanawake kutokana na wanaume kushindwa kuvumilia hali hiyo, ambapo kwa wilaya ya Sengerema zaidi ya matukio matatu yametokea kwa mwaka huu.

Na:Emmanuel Twimanye.

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 47 Katika Kitongoji cha Igalalagalilo Magharibi Kijiji cha Chamabanda Kata ya Katunguru Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza amefariki Dunia  kwa kudaiwa na  kushambuliwa na kitu chenye ncha kali na mwanaume aliyeachana naye kwa madai ya kukataa kurudiana naye. 

Akizungumzia tukio hilo Tabu  Mshimo  ambaye ni  Dada  wa  marehemu amesema  kuwa  mdogo wake Vumilia mshimo aliachana na mwanaume huyo takribani miaka mitatu  lakini cha kushangaza usiku wa kuamkia leo alifika nyumbani kwake na kumshambulia na muda  mfupi baada ya kumfikisha katika Hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema ndipo alipofariki Dunia.

Sauti ya Tabu  Mshimo dada wa marehemu akizungumzia tukio

Baadhi ya ndugu na majirani wamesikitishwa na tukio hilo na kuiomba serikali kumtafuta mtuhumiwa huyo anayedaiwa kutekeleza unyama huo na kutokomea kusikojulikana na kumchukulia hatua kali za kisheria ili kukomesha matukio hayo.

Sauti za baadhi ya ndugu na majirani

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Igalagalilo magaharibi Daudi Nkombe amekiri kutokea kwa tukio hilo na kuwaomba wanaume kuridhika na maamuzi pindi wanapoachana na wake zao.

Sauti ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Igalagalilo magaharibi Daudi Nkombe

Hata hivyo  Radio Sengerema  Fm  imemtafuta kamanda wa Polisi Mkoa wa mwanza Wilbroad Mtafungwa ili kuzungumzia tukio hilo ambapo amedai   bado haijapata taarifa za tukio hilo huku akiitaka jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi.

Sauti ya kamanda wa Polisi Mkoa wa mwanza Wilbroad Mtafungwa