Sengerema FM

Wanafunzi 300 wanakaa chini Shule ya Msingi Nyamalunda Sengerema

18 February 2024, 7:13 pm

Wanafunzi wa Darasa la nne Shule ya Msingi Nyamalunda wakiwa wamekaa chini kutokana na uhaba wa madawati shulleni hapo. Picha na Emmanuel Twimanye

Licha ya juhudi za Serkali kujenga na kukarabati baadhi ya vyumba vya madarasa Shule za mssingi nchini baadhi ya shule zinachangamoto kubwa ya Madawati halii inayo pellekea wanafunzi wa shulle hizo kukaa chiini.

Na:Emmanuel Twimanye

Wanafunzi mia tatu katika shule ya Msingi Nyamalunda  kata ya Kagunga Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wanalazimika kusoma wakiwa wamekaa chini  kutokana na shule hiyo kukabiliwa na upungufu wa madawati  kwa muda mrefu.

Changamoto hiyo imeibuliwa katika ziara ya kamati ya Sekretarieti ya chama cha mapinduzi (CCM)  Wilayani Sengerema  baada ya  kutembelea shuleni hapo  na kukuta wanafunzi wanasoma wakiwa wamekaa chini.

Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamesema kuwa wanasoma katika mazingira magumu na kwamba muda mwingine hushindwa kuelewa wanachofundishwa na walimu.

Sauti ya Wanafunzi Shule ya Msingi Nyamalunda

Mwalimu wa taaaluma katika shule  ya Msingi Nyamalunda  Mwl. Masunga Kulwa amesema kuwa changamoto hiyo imedumu kwa muda mrefu bila kutatuliwa .

Sauti ya Mwl. wa Taaluma shule  ya Msingi Nyamalunda  Mwl. Masunga Kulwa

Kufuatia hali hiyo katibu wa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Sengerema Jmal Athumani amelazimika kumpigia simu Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Sengerema Binuru Shekidele  na kuahidi kushughulikia changamoto hiyo.

Sauti ya katibu wa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Sengerema Jmal Athumani