Sengerema FM

Mwili wa kichanga waokotwa kwenye shamba la mahindi Sengerema

7 February 2024, 7:59 pm

Kituo cha polisi kilichopo kata ya Ngoma Sengerema. Picha maktaba ya Radio Sengerema

Tukio la kichanga kukutwa kimefariki kwenye Shamba la mahindi limewashangaza na kuibua hisia tofauti kwa wakazi wa kijiji cha Ngoma, ambapo mpaka sasa hawajaweza kutambua mama wa kichanga hicho.

Na; Emmanuel Twimanye

Mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miezi 8 amekutwa amefariki dunia kwenye shamba la mahindi katika kijiji cha Ngoma kata ya Igalula wilayani Sengerema mkoani Mwanza.

Baadhi ya wananchi wamesikitishwa na kulaani vikali tukio hilo la kinyama na kuiomba serikali kufanya uchunguzi ili kubaini mtu  aliyetupa mtoto huyo na kumchukulia hatua kali za kisheria.  

Sauti ya Wananchi na mashuhuda wa tukio hilo

Nao baadhi ya viongozi wa Dini  Wilayani Sengerema wamelaani vikali tukio hilo na kuiwaomba  jamii kuacha tabia ya kutupa watoto kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume na matakwa ya mwenyezi Mungu.

Sauti ya Viongozi wa Dini wakizungumzia tukio hilo

Mwenyekiti wa Kijiji cha Ngoma Sungu Mkonole   amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kuendelea kushiriana na wananachi kumtafuta mtu aliyefanya kitendo cha kikatili na kumchukulia hatua kali za kisheria.

Sauti ya Mwenyekiti wa kijiji cha Ngoma Bwn.Sungu Mkonole 

Hata hivyo Jeshi la Polisi Kituo cha Ngoma limefika eneo la tukio na kuruhusu kufanyika kwa taratibu za mazishi .