Sengerema FM

Mlinzi achinjwa na watu wasiojulikana usiku Sengerema

30 January 2024, 2:32 pm

Baadhi ya Wananchi waliofika kwenye eneo la Nchemenche mjini Sengerema kushuhudia tukio hilo.Picha na Said Mahera.

Matukio ya walinzi kuuawa mjini Sengerema yamekuwa yakijirudia mara kwa mara kila mwaka jambo hili limekuwa likihusishwa na imani za kishirikina pamoja na wivu wa kimapenzi.

Na;Said Mahera

Mtu  mmoja  anaesadikiwa  kuwa ni mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya  Mwasenda  aliyekuwa akilinda katika ukumbi wa starehe wa Nchemenche Pub uliopo mtaa wa Migombani kata ya Nyampulukano Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza,ameuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana.

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesikitishwa na mauaji hayo ya kinyama, na kuiomba serikali kufanya uchunguzi  wa  kina  kwa kushilikiana  na  jamii kuwabaini watu waliofanya kitendo hicho, na kuwachukulia hatua kali za kisheria ili kukomesha ukatili  huo.

Sauti ya Wananchi wakizungumzia tukio la mlinzi kuchinjwa na watu ambao hawajafahamika

Mmiliki wa ukumbi wa Nchemenche Sylvester Nchemenche  amesikitishwa na tukio hilo  huku  akiviomba vyombo vya dola kufanya uchunguzi  wa tukio hilo ili kubaini watu waliotekeleza unyama  huo.

Sauti ya Mmiliki wa ukumbi wa Nchemenche Sylvester Nchemenche 

Nae mwenyekiti wa mtaa wa Migombani Antony Busumabu  amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo na kutaja jina la mlinzi ambae  ameuawa kuwa ni Ghati Lioba Chacha mwenye umri wa miaka 35 .

Sauti ya mwenyekiti wa mtaa wa Migombani Antony Busumabu

Hata hivyo Jeshi la Polisi Wilayani Sengerema limefika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa marehemu kisha kuupeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali teule ya Wilaya ya Sengerema .